Rais wa Nigeria awaapisha mawaziri wapya akiwahimiza kujenga upya imani ya umma
2023-08-22 09:10:11| CRI

Rais Bola Tinubu wa Nigeria Jumatatu aliwaapisha mawaziri wapya walioteuliwa akisisitiza kazi yao muhimu katika kujenga upya imani ya umma na kuhimiza maendeleo ya nchi.

Akihutubia kwenye hafla ya kuapishwa kwa mawaziri hao iliyofanyika mjini Abuja, rais Tinubu aliwahimiza mawaziri 45 waonyeshe ustadi na ujuzi wao na kusisitiza haja ya kutatua masuala makuu ya nchi kupitia njia ya ushirikiano.

Alibainisha kuwa wajibu muhimu wa mawaziri hao ni kurejesha imani ya umma kwa serikali, ili wananchi wao waamini tena kuwa serikali yao inaweza kuwa nguvu chanya ya mageuzi na kuhimiza maendeleo ya pamoja ya wananchi. Aliongeza kuwa mawaziri hao watabeba majukumu makubwa katika kutunga sera zitakazobadilisha maisha ya watu wa Nigeria.