ECOWAS yakataa pendekezo la watawala wa Kijeshi Niger
2023-08-23 10:57:22| cri

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, imekataa pendekezo la Utawala wa Kijeshi wa Niger la kutaka kufanya uchaguzi ndani ya miaka mitatu, hatua ambayo inaweza kuongeza mvutano kama hakuna makubaliano yatakayofikiwa.

ECOWAS na wasuluhishi wengine wenye ushawishi, wamekuwa wakitafuta suluhu za kidiplomasia baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Julai 26 nchini Niger, ambayo ni ya saba katika kanda ya Afrika Magharibi na Kati, katika kipindi cha miaka mitatu.