Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa tarehe 22 Agosti walikutana na wanahabari baada ya kufanya mazungumzo katika Ikulu ya Afrika Kusini mjini Pretoria.
Xi alisema hii ni ziara yake ya nne nchini Afrika Kusini akiwa rais wa China. Mwaka huu inatimia miaka 25 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Afrika Kusini. Katika miaka hiyo 25, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepiga hatua zaidi katika maendeleo yake, hali ya kuaminiana ya kimkakati imefikia kiwango kipya, ushirikiano kwenye sekta mbalimbali umehimizwa kwa pande zote, na uratibu wa pande nyingi umekuwa wa karibu zaidi.
Xi aliongeza kuwa mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS umefunguliwa, ambao una umuhimu mkubwa katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano kwa nchi za BRICS, na kuhimiza maendeleo ya mfumo wa ushirikiano wa BRICS. Amebainisha kuwa wanataka kutia nguvu kubwa mpya kwenye maendeleo ya uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika.
Kwa upande wa Afrika Kusini, Ramaphosa alisisitiza kuwa Afrika Kusini itaendelea kuungana mkono kithabiti na China juu ya maslahi makuu na masuala makubwa yanayofuatiliwa na nchi hizo mbili.