Rais wa China atoa hotuba katika ufungaji wa baraza la biashara la nchi za BRICS
2023-08-23 09:52:22| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba yenye kichwa cha “Kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kukabiliana na changamoto na hatari, kujenga kwa pamoja dunia ya kupendeza zaidi” katika ufungaji wa baraza la biashara la nchi za BRICS uliofanyika huko Johannesburg.

Rais Xi amesema, mabadiliko ya dunia, ya zama na ya historia kwa sasa yakiendelea kwa njia ambayo haikuwahi kushuhudiwa hapo zamani. Alihoji kuwa je watu wanapaswa kushikilia ushirikiano na muungano, au kuelekea kutengana na kugongana? Je wanapaswa kushikana mikono kulinda amani na utulivu, au kuanguka katika shimo la “Vita Vipya Baridi”? Je, wanapaswa kuelekea ustawi kwa uwazi na njia shirikishi, ama kudidimia kiuchumi kwa mabavu na ubabe? Je, wanapaswa kuimarisha kuaminiana katika mawasiliano na kujifunza kwa pamoja, ama kuruhusu kiburi na ubaguzi kuzuia dhamira? Mwelekeo wa historia inaamuliwa na sisi.

Rais Xi amesisitiza, sasa dunia ni jumuiya yenye hatima ya pamoja inayoleta ustawi ama hasara kwa binadamu wote. Watu wa nchi mbalimbali wanatarajia dunia yenye amani ya kudumu, usalama wa pande zote, ustawi wa pamoja, shirikishi na uwazi, usafi na uzuri, na wala sio vita vipya baridi au kuwa na kikundi kidogo fulani. Hii ni mantiki ya maendeleo ya historia, wimbi la maendeleo ya zama. Nchi mbalimbali zinatakiwa kushikilia mitazamo sahihi kuhusu dunia, historia na hali ya jumla, na kubadilisha wazo la kujenga jumuiya yenye hatima ya pamoja ya binadamu kuwa hatua, na kufanya mustakabali kuwa uhalisia.