Kenya na Indonesia wazindua mradi wa kumiminina mafuta
2023-08-23 09:09:07| cri

Rais William Ruto na mwenzake wa Indonesia Joko Widodo wamezindua mradi wa kumimina mafuta ya kupikia kwa viwango vidogo, almaarufu Mama Pima Edible Oil Dispensing Machines ambao utasambaza mafuta kwa vipimo vidogo.

Mashine hizo za kumimina mafuta zitasambazwa na Wizara ya Viwanda.

Serikali inasema kwamba mradi huo ambao ni wa ushirikiano baina ya Kenya na Indonesia utasaidia wananchi wa pato la chini kujinunulia mafuta ya kupikia kwa bei nafuu hali kadhalika kusaidia kupatikana kwa nafasi za ajira.