Misri yathibitisha kesi mpya za virusi vya Corona vilivyobadilika
2023-08-23 10:56:49| cri

Misri imeripoti kesi mbili za kwanza za aina mpya ya virusi vya Corona vilivyobadilika vinavyoitwa EG.5.

Wizara ya Afya nchini humo imesema katika taarifa yake kuwa, kesi zote zimeonyesha dalili ndogo, na kupendekeza watu kupata chanjo ya COVID-19 ya ziada kama njia ya tahadhari.

EG.5 ni aina ya virusi vya Corona, na kesi ya kwanza iliripotiwa mwezi Februari mwaka huu.