AU yasitisha uanachama wa Niger
2023-08-23 10:04:26| CRI

Umoja wa Afrika (AU) umetoa taarifa ukilaani mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibuni nchini Niger na kuamua kusitisha uanachama wa Niger wa AU.

Taarifa hiyo imesema kuwa Baraza la Amani na Usalama la AU hivi karibuni limekutana kujadili hali ya Niger, likilaani mapinduzi yaliyotokea tarehe 26 mwezi Julai, na kulitaka jeshi la Niger kuweka maslahi ya nchi na watu mbele na kurejea kwenye kambi zao za kijeshi mara moja bila masharti.

Taarifa hiyo imesema kuwa Baraza la Amani na Usalama la AU limeamua kusitisha mara moja ushiriki wa Niger katika shughuli zote za AU na taasisi zake hadi nchi hiyo itakaporejesha kikamilifu utaratibu wa kikatiba.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa AU inaunga mkono kikamilifu juhudi zinazoendelea za Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kurejesha utulivu wa kikatiba nchini Niger kwa njia za kidiplomasia.