CMG na SABC kushirikiana kutengeneza filamu za documentary
2023-08-24 10:34:35| cri

Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini SABC jana Agosti 23 walitangaza kushirikiana katika kutengeneza filamu za documentary kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini katika miaka 25 iliyopita.

Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong na Mwakilishi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa SABC Bibi Yolande van Biljon ambaye ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa SABC, waliwasha kamera kwa pamoja kwa ajili ya utengenezaji wa filamu hizo, na pia wameshuhudia kubadilishana kwa nyaraka za ushirikiano.

Bw. Shen Haixiong amesema anatumai pande hizo mbili zitatumia vizuri fursa hii kuendelea kutafuta njia mpya ya ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote, ili kutoa mchango zaidi katika kuzidisha maelewano kati ya watu wa China na Afrika Kusini na kufundishana kati ya staarabu za nchi hizo mbili.