Watoto 500 wafariki kwa njaa Sudan mapigano yakiendelea
2023-08-24 10:42:07| cri

Shirika la Kimataifa la Hisani la Save the Children limesema, tangu mapigano yalipozuka nchini Sudan mwezi Aprili, watoto 500 wamefariki kutokana na njaa, wakiwemo watoto zaidi ya 20 katika kituo cha watoto yatima kinachosimamiwa na serikali katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum,.

Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Sudan, Arif Noor amesema, idadi ya watoto walioachishwa shule nchini Sudan pia imeongeza, na kwamba karibu watoto 31,000 wanakosa huduma ya lishe na matibabu ya utapiamlo tangu Shirika hilo lilipositisha shughuli zake kwenye vituo 57 vya lishe nchini Sudan.

Mapigano yanayoendelea nchini Sudan, umegeuza jiji la Khartoum na maeneo mengine ya mijini kuwa viwanja vya vita huku wakazi wengi wakiishi bila maji na umeme, na mfumo wa huduma za afya nchini humo umeharibika.