Viongozi wa nchi za BRICS wahimiza kuimarisha ushirikiano wa sekta mbalimbali na kulinda mfumo wa pande nyingi
2023-08-24 09:45:10| CRI

Mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za BRICS umefanyika huko Johannesburg. Viongozi wa nchi za BRICS wametoa hotuba katika mkutano huo, huku wakitoa mwito wa kuimarisha ushirkiano wa uchumi, bishara na fedha, kupanua ushirikiano wa usalama wa kisiasa, kuimarisha mawasiliano ya utamaduni, kuboresha mfumo wa utawala wa dunia nzima na kulinda hali yenye pande nyingi.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa nchi za BRICS ametoa hotuba akisema, katika miongo kadhaa iliyopita, nchi za BRICS siku zote zimekuwa nguvu kuu ya kuhimiza ukuaji wa uchumi, biashara na uwekezaji wa dunia. Nchi za BRICS zinapendekeza ushirikishi na kuhimiza kujenga utaratibu wa dunia wenye usawa na haki zaidi.

Katika hotuba yake, rais Lula da Silva wa Brazil amesema katika miaka kadhaa iliyopita, dunia imerudi nyuma kutoka hali nzuri yenye ncha nyingi hadi hali ya kurejesha vita baridi na ushindani wa siasa za kijiografia ambayo imepitwa na wakati, na hii italeta hali ya sintofahamu na kuharibu hali yenye pande nyingi, ambapo hatari zilizomo ndani haziwezi kukubaliwa na binadamu.

Siku hiyohiyo rais Vladimir Putin wa Russia ametoa hotuba kupitia njia ya video akisema, nchi za BRICS zinaongeza uwezo wao mwaka baada ya mwaka, na imekuwa mfumo muhimu katika jukwaa la kimataifa ikiwa na ushawishi unaozidi kuongezeka katika mambo ya kimataifa. Jambo muhimu zaidi ni kwamba nchi za BRICS zinakubaliana kuanzisha utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi wenye haki halisi na ulio katika msingi wa sheria za kimataifa na kufuata katiba ya Umoja wa Mataifa na kupinga umwamba wa aina yoyote.

Kwa upande wa waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi, amesema kuwa katika miongo miwili iliyopita, nchi za BRICS zimepata mafanikio mengi, Benki ya Maendeleo Mapya imetoa umuhimu wake katika maendeleo ya nchi za kusini. Kupitia hatua mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa usafiri wa anga ya juu, uzinduzi wa kituo cha utafiti cha chanjo, mfumo wa ushirikiano wa nchi za BRICS umeleta mabadiliko chanya kwa maisha ya watu wa kawaida wa nchi hizo. Modi pia amesema, India inaunga mkono kwa juhudi iwezavyo BRICS kupanua uanachama wake, na kukaribisha maafikiano na maendeleo husika kupatikana.