Nchi 6 zaalikwa kujiunga na BRICS
2023-08-24 21:47:44| cri

Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika asubuhi ya Agosti 24, kwa saa za Afrika Kusini, viongozi wa nchi za kundi la BRICS wametangaza mpango wa upanuzi wa uanachama wa kundi hilo. Nchi 6 zikiwemo Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Falme za Kiarabu zimealikwa kujiunga na kundi hilo.