Watu wawili wauawa katika shambulio linakisiwa kufanywa na kundi la Al-Shabaab nchini Kenya
2023-08-24 23:40:59| cri

Dereva wa lori na dereva msaidizi wameuawa jana asubuhi kufuatia shambulio la ghafla lililofanywa na watu waliokuwa na silaha nzito wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab karibu na eneo la Lango la Simba kwenye barabara ya Lamu-Witu-Garsen nchini Kenya.

Naibu kamishna wa Kaunti ya Lamu Gabriel Kioni amesema, awali, magaidi hao walichoma moto nyumba nane na kanisa katika kijiji cha Salama kilichoko Lamu Magharibi usiku wa kuamkia jumanne. Ameongeza kuwa, jumatatu usiku, magaidi hao waliiba vitu mbalimbali katika vijiji vya eneo hilo, ikiweno luninga, paneli za umeme wa jua, taa, unga wa mahindi na mbuzi.