Biashara kati ya China na Afrika yaongezeka kwa utulivu katika kipindi cha miezi saba ya mwanzo ya mwaka huu
2023-08-24 10:39:04| cri

Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Forodha ya China zimeonyesha kuwa, biashara kati ya China na Afrika imeongezeka kwa utulivu katika miezi saba ya mwanzo ya mwaka huu.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka kwa asilimia 7.4 katika kipindi hicho ikilinganishwa na mwaka jana, na kufikia dola za kimarekani bilioni 158.36.

China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa wa biashara wa Afrika, na biashara kati ya pande hizo mbili ilifikia dola za kimarekani trilioni 0.26 ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.8 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2021.