CMG na Shirikisho la Soka la Afrika Kusini zafanya ushirikiano na mawasiliano
2023-08-24 09:45:44| CRI

Wakati rais Xi Jinping wa China akihudhuria mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi za BRICS na kufanya ziara ya kitaifa nchini Afrika Ksuini, ili kuzidisha utekelezaji wa makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais wa nchi mbili, Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Shirikisho la Soka la Afrika Kusini yamebadilishana nyaraka za ushirikiano. Pande mbili zimefikia makubaliano kuhusu kuimarisha mawasiliano ya utamaduni wa soka na mechi za soka, ushirikiano wa matangazo ya televisheni ya mechi za soka, na  mawasiliano ya watu.

Mkuu wa Shirika la CMG Bw. Shen Haixiong amesema, michezo ni lugha ya pamoja ya binadamu na mawasiliano ya michezo ni sehemu muhimu ya mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika Kusini. Mafanikio ya Kombe la dunia la 2010 lililofanyika nchini Afrika Kusini limeweka kumbukumbu nyingi na kuibua shauku ya mashabiki wa soka wa China, ambayo imekuwa na maana kubwa katika kueneza utamaduni wa Soka na kuonesha taswira ya Afrika Kusini mpya.

Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika Kusini Dkt Danny Jordaan amepongeza mafanikio yaliyopatikana na China katika ujenzi wa mambo ya michezo, huku akisifu rekodi kadhaa zilizowekwa za utazamaji wa mechi za kombe la dunia la mwaka 2010 kupitia channeli za CCTV.