China yaikabidhi Sudan Kusini kituo cha kisasa cha utangazaji
2023-08-24 09:44:24| CRI

Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umeikabidhi nchi hiyo kituo cha kisasa cha utangazaji huko mjini Juba, mji mkuu wa nchi hiyo, ili kusaidia kuimarisha huduma za utangazaji wa kidijitali nchini humo.

Kituo hicho kinachosaidiwa na China kina jengo jipya la studio ya utayarishaji wa vipindi vya TV, linalochukua eneo la takriban mita za mraba 2,400. Kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Waziri wa Habari, Mawasiliano, Teknolojia na Huduma za Posta wa Sudan Kusini Bw. Michael Makuei Lueth amesema kuwa makabidhiano ya kiufundi ya vifaa hivyo yatawezesha wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC) kupata mafunzo ya wasimamizi kamili na wadhibiti wa vifaa.

Balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Ma Qiang amesema kuwa wafanyakazi 726 wa Sudan Kusini na wenzao 127 wa China walishiriki katika ujenzi wa kituo hicho. Na tasnia ya utangazaji na TV ina jukumu muhimu katika jamii ya kisasa, na kuchangia maendeleo ya kiuchumi, ustawi wa kitamaduni, maendeleo ya kiufundi na furaha ya taifa.