Rais Xi asema China ya kisasa italeta fursa mpya kwenye ushirikiano kati ya China na Ethiopia
2023-08-24 09:43:43| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema China inaendeleza China ya kisasa kwa maendeleo yake ya hali ya juu, jambo ambalo litaleta fursa mpya za ushirikiano kati ya China na Ethiopia.

Rais Xi ameyasema hayo alipokutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kando ya Mkutano wa kilele wa 15 wa BRICS, akisistiza kuwa China ni rafiki wa kutegemewa na mshirika wa kweli wa Ethiopia. Amebainisha kuwa katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimedumisha mabadilishano na mawasiliano ya mara kwa mara ya kiwango cha juu, na zimepata matokeo ndani ya mifumo ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja Njia Moja na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

Wakati huohuo rais Xi pia alikutana na mwenzake wa Senegal Macky Sall kando ya mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za BRICS, Akisema kuwa Senegal ni mshirika muhimu wa China barani Afrika, na kutokana na juhudi za pamoja katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimekuwa na hali ya kina ya kuaminiana kisiasa na ushirikiano wenye manufaa katika nyanja mbalimbali.

Xi amebainisha kuwa China inaunga mkono kithabiti juhudi za Senegal katika kulinda utulivu na maendeleo ya taifa, na kuongeza kuwa China iko tayari kuimarisha uungaji mkono wa pande zote na Senegal na kuzidisha ushirikiano katika maeneo kama vile viwanda, kilimo, miundombinu na rasilimali watu, kulinda kwa pamoja haki yao halali ya maendeleo, na kusukuma mbele zaidi maendeleo ya ushirikiano wao wa wa kina wa kimkakati.