Rais wa Afrika Kusini aonya dhidi ya hatua za kujilinda na upande mmoja
2023-08-24 10:39:47| cri

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa jana jumanne ameonya dhidi ya wimbi jipya la kujilinda na athari za hatua za upande mmoja, na kutoa wito wa uwazi na ujumuishi ili kulinda ukuaji wa uchumi.

Akizungumza katika Jukwaa la Majadiliano ya Biashara ya Viongozi wa BRICS mjini Johannesburg, Afrika Kusini, rais Ramaphosa amesema nchi za BRICS zimeibuka na kuwa injini ya nguvu kwa ukuaji wa uchumi wa dunia, na mabadiliko yaliyotokea kwenye nchi hizo katika muongo mmoja uliopita yamefanya mambo mengi katika mageuzi ya muundo wa uchumi wa dunia.

Amesema thamani ya jumla ya biashara kati ya nchi wanachama wa BRICS imefikia dola za kimarekani bilioni 162 mwaka 2022, na kusisitiza umuhimu wa nafasi ya uwekezaji wa kigeni katika ukuaji wa uchumi wa nchi za BRICS.