Marais wa China na Russia wakutana
2024-07-04 08:41:12| CRI

Rais Xi Jinping wa China amekutana na rais Vladimir Putin wa Russia jana Jumatano, huko Astana, Kazakhstan, kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai (SCO).

Rais Xi amesisitiza kuwa, China na Russia zinapaswa kuendelea kuimarisha uunganishaji wa mikakati ya maendeleo na ushirikiano wa kimkakati wa kimataifa. Amesema China inaunga mkono Russia kutekeleza majukumu ikiwa mwenyekiti wa zamu wa nchi za BRICS, kuunganisha “Dunia ya Kusini”, kuzuia “Vita Mpya ya Baridi”, na kupambana na vikwazo visivyo halali vinavyotekelezwa na upande mmoja. Pia amesisitiza kuwa China inatarajia kushirikiana na Russia na nchi nyingine wanachama wa SCO kuijenga kuwa jumuiya ya pamoja ambayo ina uhusiano wa karibu zaidi.

Kwa upande wake rais Putin amesema Russia inaunga mkono China kulinda maslahi yake kuu na haki halali, na kupinga nguvu za nje kuingilia kati mambo ya ndani ya China na suala lake la Bahari ya Kusini. Pia amesisitiza kuwa China itachukua nafasi ya uwenyekiti mpya wa zamu wa SCO, na kwamba Russia itaunga mkono kikamilifu kazi ya China, na kushirikiana na nchi nyingine wanachama ili kulinda amani na usalama wa kanda hiyo, na kuhimiza mfumo wa kimataifa kuelekea kwa upande wa haki na usawa zaidi.