Xi asema China yapenda kusukuma mbele uhusiano na Poland hadi kufikia kiwango cha juu
2024-06-25 09:08:59| CRI

Rais wa China Xi Jinping Jumatatu ameeleza nia ya China ya kushirikiana na Poland katika kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili ili kufikia kiwango cha juu na kuleta utulivu na uhakika zaidi katika dunia yenye misukosuko.

Xi ameyasema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo mjini Beijing na Rais wa Poland Andrzej Duda ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China. Akibainisha kuwa Poland ni moja ya nchi za kwanza kuitambua Jamhuri ya Watu wa China, Xi alisema uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedumisha maendeleo thabiti tangu nchi hizo mbili zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 75 iliyopita.

Tangu China na Poland zianze kuboresha uhusiano wao na kufikia ushirikiano wa kimkakati miaka minane iliyopita, mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali umepanuka na kuimarika kwa pande zote, na kunufaisha watu wa pande mbili.

Kwa upande wake Duda alisema Poland inapenda kudumisha mawasiliano ya karibu na uratibu wa pande nyingi na China ili kuendeleza zaidi ushirikiano wao wa kimkakati wa kina na kuchangia amani na utulivu wa dunia.

Pande hizo mbili pia zilibadilishana mawazo kuhusu mzozo wa Ukraine.