Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), katika operesheni yao ya pamoja iliyofanyika mashariki mwa DRC, yamewaokoa watu 30 waliotekwa na waasi wa kundi la ADF.
Katika taarifa yake, msemaji wa Jeshi la Uganda katika eneo la Mlimani, Maj. Bilal Katamba, amesema watu hao waliookolewa walipelekwa katika kambi ya Jeshi la DRC iliyoko Erengeti, mkoa wa Kivu Kaskazini jumanne wiki hii.
Amesema operesheni hiyo ya pamoja ya majeshi hayo dhidi ya waasi wa kundi la ADF katika eneo la mashariki mwa DRC imewezesha kuokolewa kwa watu waliotekwa nyara, kukamata silaha, na vifo vya waasi hao.