Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba Agtosti 23 kwenye mkutano wa 15 wa Kilele wa kundi la BRICS uliofanyika Johannesbrug, nchini Afrika Kusini, akitoa wito la kuzidisha ushirikiano wa kundi hilo na kuongeza usawa na haki duniani.
2023-08-25 09:43:27| cri

KUTAFUTA MAENDELEO KUPITIA MSHIKAMANO NA USHIRIKIANO, NA KUBEBA WAJIBU WETU KWA AMANI

Mheshimiwa Rais Matamela Cyril Ramaphosa,

Mheshimiwa Rais Luiz Inacio Lula da Silva,

Mheshimiwa Rais Vladimir Putin,

Mheshimiwa Waziri Mkuu Narendra Modi,

Nina furaha kubwa sana kuungana nanyi hapa Johannesburg kwenye mijadala muhimu kuhusu ushirikiano na maendeleo ya kundi la BRICS. Ni muhimu zaidi kwamba Mkutano wa kilele wa kundi la BRICS unafanyika barani Afrika kwa mara ya tatu. Ningependa kumshukuru Rais Ramaphosa na serikali ya Afrika Kusini kwa maandalizi mazuri.

Tunakutaka hapa wakati dunia imeingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko. Wakati inapitia mabadiliko makubwa, mgawanyiko na kujiunda upya, na kusababisha maendeleo yasiyo ya uhakika, yasiyo na utulivu, na yasiyotabirika.

Kundi la BRICS ni nguvu muhimu katika kujenga mazingira ya kimataifa. Tunachagua njia zetu za maendeleo kwa kujitegemea, tunatetea kwa pamoja haki yetu ya maendeleo, na kuandamana kwa pamoja kuelekea mambo ya kisasa. Hii inawakilisha mwelekeo wa maendeleo ya jamii ya wanadamu, na itaathiri sana mchakato wa maendeleo ya ulimwengu. Rekodi yetu ya utendaji inaonesha kwamba tumeendelea kufanya kazi kulingana na roho ya BRICS ya uwazi, ushirikishwaji na ushirikiano wa kunufuishana, na kuinua ushirikiano wa BRICS kwa viwango vipya ili kuunga mkono maendeleo ya nchi zetu tano. Tumedumisha haki na usawa kwenye masuala ya kimataifa, tumesimamia kilicho haki kwenye masuala makubwa ya kikanda na kimataifa, na kuimarisha sauti na ushawishi wa nchi zinazoibukia na zinazoendelea. Nchi za BRICS daima zinatetea na kutekeleza sera huru ya mambo ya nje. Kila mara tunashughulikia masuala makuu ya kimataifa kulingana na hali halisi, kutoa maoni ya haki na kuchukua hatua za haki. Hatubadilishi kanuni, hatusujudu mbele ya shinikizo la nje, au kuwa vibaraka wa wengine. Sisi nchi za BRICS tunashiriki makubaliano ya kina na malengo ya pamoja. Haijalishi jinsi gani hali ya kimataifa inavyobadilika, ahadi yetu ya ushirikiano tangu mwanzo na matarajio yetu ya pamoja havitabadilika.

Tunakutanaa katika wakati muhimu ili kuendeleza mafanikio yetu ya zamani na kufungua mustakabali mpya wa ushirikiano wa kundi la BRICS. Tunapaswa kufuata mwenendo wa nyakati zetu na kuwa mstari wa mbele. Daima tunapaswa kukumbuka madhumuni yetu ya msingi ya kujiimarisha kupitia umoja, kuimarisha ushirikiano kote duniani, na kujenga ushirikiano wa hali ya juu. Tunapaswa kusaidia mageuzi ya usimamizi wa dunia ili kuufanya uwe wa haki zaidi na usawa, na kuleta uhakika zaidi duniani, utulivu na hali chanya.

-Tunapaswa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kifedha ili kukuza ukuaji wa uchumi. Maendeleo ni haki isiyotengeka ya nchi zote, na si fursa maalum kwa watu wachache. Kuimarika kwa uchumi wa dunia bado kunatetereka, huku kukiwa na chini ya asilimia tatu ya ukuaji kwa mwaka kama inavyokadiriwa na baadhi ya taasisi za kimataifa. Changamoto kwa nchi zinazoendelea ni kubwa zaidi, ambazo zinakwamisha juhudi zetu za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. Sisi nchi za BRICS tunapaswa kuwa washirika katika safari ya maendeleo na ufufuaji wa uchumi, na kupinga kuzorotesha na kukatika minyororo ya ugavi, pamoja na ushurutishaji wa kiuchumi. Tunapaswa kuzingatia ushirikiano kivitendo, hasa katika nyanja za uchumi wa kidijitali, maendeleo yasiyosababisha uchafuzi na ugavi, na kuimarisha mabadilishano ya kiuchumi, biashara na kifedha.

China itaanzisha Eneo la Kukuza Sayansi na Uvumbuzi la China na BRICS kwa zama mpya ili kuunga mkono matumizi ya matokeo ya uvumbuzi wa kisayansi. Chini ya utaratibu wa Makundi ya satelaiti za utambuzi kutoka mbali wa nchi za BRICS, tutachunguza uanzishwaji wa Jukwaa la data za satelaiti za utamubuzi kutoka mbali na matumizi ya data hizo duniani kwa ushirikiano la BRICS, ili kutoa uungaji mkono wa data kwa ajili ya kilimo, uhifadhi wa ikolojia na kupunguza majanga katika nchi mbalimbali. China pia itashirikiana na pande zote ili kuanzisha kwa pamoja Mfumo wa BRICS wa Ushirikiano wa Viwanda kwa Maendeleo Endelevu, likiwa ni jukwaa la uratibu wa viwanda na ushirikiano wa miradi katika kutekeleza Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa.

-Tunapaswa kupanua ushirikiano wa kisiasa na usalama ili kudumisha amani na utulivu. Kama msemo wa Wachina unavyosema, "Hakuna chenye manufaa zaidi kuliko utulivu, na hakuna kinachodhuru zaidi kuliko msukosuko." Mtazamo wa Vita Baridi bado unasumbua dunia yetu, na hali ya siasa za kijiografia inazidi kuwa mbaya. Nchi zote zinatamani mazingira mazuri ya usalama. Usalama wa kimataifa haugawanyiki. Majaribio ya kutafuta usalama kamili kwa gharama ya wengine hatimaye yataleta matokeo mabaya. Mgogoro wa Ukraine umebadilika hadi kuwa ulivyo sasa kutokana na sababu zenye utatanishi. Cha muhimu kwa sasa ni kuhimiza mazungumzo ya amani, kukuza kupunguza mgogoro, kumaliza mapigano na kufikia amani. Hakuna mtu anayepaswa kuongeza mafuta kwenye moto ili kufanya hali izidi kuwa mbaya.

Nchi za BRICS zinapaswa kuzingatia mwelekeo wa maendeleo ya amani na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa BRICS. Tunahitaji kutumia vyema Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa BRICS, Mkutano wa Wawakilishi Wakuu wa Usalama wa Taifa na mifumo mingine, kusaidiana katika masuala yanayohusu maslahi yetu ya msingi, na kuimarisha uratibu katika masuala makuu ya kimataifa na kikanda. Tunahitaji kujitahidi kushiriki kwenye utatuzi wa masuala yenye utatanishi, kuhimiza suluhu la kisiasa na kupunguza migogoro. Akili bandia (AI) ni eneo jipya la maendeleo. Nchi za BRICS zimekubaliana kuzindua Kikundi cha Utafiti cha Akili Bandia cha Taasisi ya Mitandao ya Baadaye ya BRICS katika siku zijazo. Tunahitaji kuwezesha Kikundi cha Utafiti kutekeleza jukumu lake kikamilifu, kupanua zaidi ushirikiano kwenye Akili Bandia, na kuongeza kasi ya kubadilishana taarifa na ushirikiano wa kiteknolojia. Tunahitaji kwa pamoja kuzuia hatari, na kukuza mifumo na viwango vya usimamizi wa Akili Bandia kwa maafikiano mapana, ili kufanya teknolojia za Akili Bandia kuwa salama zaidi, zinazotegemewa, kudhibitiwa na usawa.

-Tunapaswa kuongeza mawasiliano kati ya watu na kuhimiza kujifunza kwa wengine kati ya staarabu. Kuna staarabu nyingi na njia nyingi za maendeleo duniani, na hivi ndivyo dunia inavyopaswa kuwa. Historia ya binadamu haitaisha kwa ustaarabu au mfumo fulani. Nchi za BRICS zinahitaji kutetea ari ya ujumuishaji, kutetea kuishi pamoja kwa amani na hali ya masikilizano kati ya staarabu, na kuheshimu njia iliyoamuliwa na nchi moja moja katika ujenzi wa nchi ya kisasa. Tunahitaji kutumia vyema mbinu kama vile semina ya BRICS kuhusu utawala, kongamano la BRICS kuhusu mawasiliano ya watu na mabadilishano ya kitamaduni, na Shindano la Ubunifu la Wanawake ili kuongeza mawasiliano kati ya watu na kuimarisha uhusiano kati ya watu wetu.

China inapendekeza kwamba nchi za BRICS zipanue ushirikiano katika elimu, kuongeza nafasi ya ushirikiano wa BRICS wa elimu ya ufundi stadi, kuchunguza na kuweka utaratibu wa ushirikiano kuhusu elimu ya kidigitali, na kuhimiza dhana ya ushirikiano wa pande zote kuhusu elimu. Zaidi ya hayo, tunahitaji pia kuimarisha mabadilishano kuhusu tamaduni za jadi na kuhimiza kuendeleza tamaduni bora za jadi.

-Tunapaswa kuzingatia usawa na haki, na kuboresha usimamizi wa kimataifa. Kuimarisha usimamizi wa dunia ni chaguo sahihi ikiwa jumuiya ya kimataifa inakusudia kuchangia fursa za maendeleo na kukabiliana na changamoto za kimataifa. Kanuni za kimataifa lazima ziandikwe na kuzingatiwa kwa pamoja na nchi zote kwa kuzingatia madhumuni na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, badala ya kuamriwa na wenye nguvu au wenye sauti zaidi. Kuungana ili kuwa na vikundi vya kipekee na kuzifanya sheria zao kuwa kanuni za kimataifa, ni jambo lisilokubalika. Nchi za BRICS zinapaswa kutumia mfumo kweli wa pande nyingi, kushikilia mfumo wa kimataifa unaozingatia Umoja wa Mataifa, kuunga mkono na kuimarisha mfumo wa biashara wa pande nyingi unaozingatia WTO, na kukataa jaribio la kuunda duru ndogo au kambi za kipekee. Tunahitaji kutumia kikamilifu jukumu la Benki Mpya ya Maendeleo, kusukuma mbele mageuzi ya mifumo ya kimataifa ya fedha na sarafu, na kuongeza uwakilishi na sauti ya nchi zinazoendelea.

Ninafurahi kuona hamasa inayoongezeka ya nchi zinazoendelea kuhusu ushirikiano wa BRICS, na idadi kubwa ya nchi zimetuma maombi ya kujiunga na utaratibu wa ushirikiano wa BRICS. Tunahitaji kuchukua hatua kwa moyo wa BRICS wa uwazi, ushirikishwaji na ushirikiano wa kunufaishana kuzileta nchi nyingi zaidi katika familia ya BRICS, ili kuunganisha hekima na nguvu zetu na kufanya usimamizi wa dunia kuwa wa haki na usawa zaidi.

Viongozi wenzangu,

Bara la kale la Afrika ni hifadhi ya hekima rahisi lakini ya kina. Kama msemo wa Kiafrika unavyosema, "Ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako, ukitaka kwenda mbali, nenda na wenzako." Falsafa ya Ubuntu, ambayo inaamini kwamba "Niko kwa sababu tuko," inazingatia kutegemeana na kuungana kwa watu wote. Vile vile, kuishi pamoja kwa usawa imekuwa matarajio ya taifa la China kwa maelfu ya miaka. China iko tayari kufanya kazi na washirika wa BRICS ili kufuata mtazamo wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, na kuimarisha ushirikiano wa pande zote. Kama wanachama wenzetu wa BRICS, tunapaswa kukabiliana na changamoto zetu za kawaida kwa mtazamo wa pamoja wa dhamira, kujenga maisha bora ya baadaye yenye madhumuni ya pamoja, na tuambatane pamoja katika safari ya kuelekea kuleta mambo ya kisasa.

Asanteni