Rais wa China ahudhuria mkutano maalumu na wanahabari wa mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za BRICS
2023-08-25 09:13:58| CRI

Rais Xi Jinping wa China amehudhuria mkutano maalumu na wanahabari wa mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za BRICS uliofanyika huko Johannesburg.

Mkutano huo umetangaza kuzialika Saudi Arabia, Misri, UAE, Argentina, Iran na Ethiopia kuwa wanachama wa familia ya BRICS.
Rais Xi ametoa hotuba muhimu akisema, nchi za BRICS ni nchi zenye ushawishi mkubwa, na kubeba majukumu muhimu kwa amani na maendeleo ya dunia. Katika mkutano huo, wamefanya mazungumzo ya kina kuhusu masuala kadhaa yakiwemo hali ya kimataifa, na ushirikiano wa nchi za BRICS, na kufikia makubaliano ya pamoja, huku wakitoa azimio la mkutano wa wakuu na kupata mafanikio mengi.

Rais Xi amesema, wakuu wa nchi tano wamekubaliana kuzialika nchi hizo kuwa wanachama wa familia ya BRICS. China inatoa pongezi kwa nchi hizo na kupongeza juhudi zilizofanywa na nchi mwenyekiti Afrika Kusini na rais wake Cyril Ramaphosa.