Mkuu wa jeshi la Sudan atembelea kambi za jeshi mjini Omdurman
2023-08-25 10:27:30| cri

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, jana alhamis amefanya ziara ya ukaguzi katika maeneo kadhaa ya kijeshi katika mji wa Omdurman, kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Picha na vipande vya picha za video zilizotumwa kwenye ukurasa wa Jeshi hilo katika mtandao wa Facebook zimemwonyesha Jenerali Al-Burhan akisalimiana na askari wake katika eneo la kijeshi la Wadi Seida lililoko mjini Omdurman. Jeshi hilo pia limetuma picha zikimwonyesha Jenerali Al-Burhan akisalimiana na kuongea na raia wa eneo hilo.