Wakulima nchini Tanzania kupewa bima ya afya ilikujikimu kimaisha na kibiashara
2023-08-25 23:30:04| cri

Halmashauri ya Ruangwa, mkoani Lindi huko Tanzania inatarajia kuanza kwa mchakato wa kuwakatia bima ya afya wakulima wake katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili wapate huduma hiyo kwa uharaka na kukuza tija katika ufanyaji kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Frank Chonya katika maonesho ya wiki ya madini na uwekezaji yanayo fanyika katika viwanja vya  soko jipya maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi, Irene Kataraiya ametoa rai kwa wakulima na wananchi kujitokeza kwa wingi kukata bima hiyo kwa manufaa yao wenyewe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagi akiongea katika maonyesho hayo amewaomba NHIF wayafikie makundi mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini.

Mayasa Goloa, mkazi wa Ruangwa amesema kuwa Serikali ikiamua kukata fedha moja kwa moja kwa mkulima baada ya kuuza mazao itakuwa vizuri zaidi kwasababu wengi hujisahau wakishapata fedha.