Kenya yaongoza kuwavutia watalii Afrika
2023-08-26 23:31:07| cri

Idadi ya watalii walioingia nchini kipindi cha January hadi Juni 2023 imeongezeka hadi kufikia 759,327, huku Kenya ikiongoza kutoa watalii wengi wanaotembelea Tanzania wakitokea nchi za Afrika.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu za Kiuchumi nchini Tanzania, Daniel Masolwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Mtakwimu huyo, amesema kuwa Kenya imeleta jumla ya 93,488; huku nchi zingine ambazo wananchi wake wameitembelea Tanzania katika kipindi hicho na idadi yao katika mabano ni pamoja na Burundi (47,418), Rwanda (26,899), Zambia (25, 372) na Uganda (20,727).

Hata hivyo, Masolwa amesema kuwa japo Kenya inaongoza kwa nchi za Afrika, wengi wa watalii hao ametaka nje ya bara la Afrika, huku ongezeko hilo ambalo ni sawa na asilimia 31.9; ni zaidi ya watalii 575,397 walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2022.