Msomi wa Mali: Nchi za BRICS zina nia ya pamoja ya kuunga mkono maendeleo ya Afrika
2023-08-28 09:28:58| CRI

Mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi za BRICS uliofanyika hivi karibuni huko Johannesburg nchini Afrika Kusini umeamua kuzialika Saudi Arabia, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Argentina, Iran na Ethiopia kujiunga na BRICS kama wanachama wapya, na pia umezikaribisha nchi nyingine zinazoendelea zenye nia na zilizotimiza vigezo kuwa nchi washirika wa BRICS. Upanuzi huo wa BRICS umezitia moyo nchi zote za Kusini duniani. Msomi wa Mali Prof. Yoro Diallo alipohojiwa hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), amesema nchi nyingi zimezidi kuvutiwa na mfumo wa BRICS, ambapo nchi za BRICS zinasukuma mbele mageuzi ya mfumo wa usimamizi duniani, kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja kwa njia chanya, hatua ambayo inaendana na matarajio ya watu wa nchi nyingi zinazoendelea.

 

Mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang Prof. Yoro Diallo amesema, tangu mwaka 2006, nchi za BRICS zimekuwa nguvu chanya, tulivu na ya kiujenzi, huku ushawishi wake ukizidi kupanda na kuhusiana kwa karibu na mustakbali wa nchi zinazoendelea. Nchi za BRICS zina kila sababu ya kujivunia mafanikio yaliyopatikana hasa katika ushirikiano unaohusisha nyanja za uchumi na biashara, nishati, mabadiliko ya tabianchi, na usimamizi duniani, akitolea mfano wa kuanzishwa kwa Benki Mpya ya Maendeleo ya BRICS na kukutaja kuwa ni jambo kubwa katika usimamizi wa kifedha duniani. Prof. Diallo anaona nchi za BRICS zimethibitisha uwezo wake wa kutoa suluhisho mwafaka kwa changamoto zinazoikabili dunia.

 

Prof. Diallo anaona, kaulimbinu ya mkutano huo wa BRICS ambayo ni “BRICS na Afrika: Kuimarisha Ushirikiano wa Kiwenzi, Kuhimiza Ukuaji wa Pamoja, Kutimiza Maendeleo Endelevu, Kuongeza Ushirikishi katika Mfumo wa Pande Nyingi”, inaonesha kuwa nchi za BRICS zina nia ya pamoja ya kuunga mkono maendeleo ya Afrika, na zinatarajia kuisukuma mbele Afrika kwenye njia ya kuelekea maendeleo endelevu na ustawi wa pamoja. Nchi za BRICS kupanua ushirikiano na nchi za BRICS, kutatoa mchango mkubwa zaidi kwa amani na maendeleo duniani. Amesema kwa upande wa nchi za Afrika, kuimarisha ushirikiano na nchi za BRICS kutapiga jeki maendeleo ya Afrika, na kutoa uungaji mkono muhimu kwa Afrika kutimiza Ajenda ya 2063, kuharakisha maendeleo ya kilimo, viwanda, miundombinu na uvumbuzi wa kisayansi.