Kundi la NCBA la Kenya lasema ukuaji wa biashara kati ya China na Afrika umesababisha ongezeko la akaunti za saafu ya China
2023-08-28 08:43:04| CRI

Taasisi ya huduma za kifedha nchini Kenya NCBA imesema kuwa kuongezeka kwa biashara kati ya China na Afrika kumechochea matumizi ya akaunti za sarafu ya China, Yuan.

Mkurugenzi mtendaji wa NCBA John Gachora amesema kuwa wateja wake wanaweza kufungua akaunti ya Yuan kutokana na kuwa ina mawasiliano na benki za nchini China.

Gachora amesema upatikanaji wa sarafu ya China umeleta urahisi kwa biashara kati ya China na Afrika.

NCBA inafanya kazi nchini Kenya na nchi nyingine nne za Afrika ambazo ni Uganda, Tanzania, Rwanda na Cote d’Ivoire.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya, China imekuwa mshirika mkubwa wa biashara wa nchi hiyo, mwekezaji wa kigeni na mkandarasi wa miradi mbalimbali.