Mtaalam wa Ethiopia asema hatua ya nchi hiyo kujiunga na BRICS itasaidia kuibua uchumi wa nchi hiyo
2023-08-28 08:44:49| CRI

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Huduma za Jamii nchini Ethiopia Mukerrim Miftah amesema, hatua ya nchi hiyo kujiunga na BRICS inatarajiwa kuchochea kidhahiri ukuaji wa uchumi na kuimarisha manufaa yake katika uhusiano wa kikanda.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Miftah amesema hatua hii ni msingi kwa sababu kadhaa, ikiwemo kuisaidia Ethiopia kuunda ushirikiano wa nguvu wa kiuchumi na kisiasa na nchi wanachama wa BRICS, kusaidia uhusiano mzuri wa uchumi, biashara na uwekezaji kati yake na nchi mpya na zilizopo katika kundi la BRICS.

Amesisitiza kuwa uanachama wa Ethiopia katika BRICS utawezesha nchi hiyo kuendeleza uhusiano wa kigeni katika njia ya kitaasisi zaidi na ya kunufaishana.