Mchumi wa Ghana asema, China yatoa mchango katika kusitisha madeni kwa nchi za Afrika
2023-08-28 08:44:10| CRI

Mchumi kutoka Shirika la Ushauri la Simba la nchini Ghana, Richard Dei-Tutu amesema, China imetoa mchango mkubwa katika kusitisha madeni na misaada kwa nchi za Afrika.

Alipohojiwa na Shirika la Habari la China Xinhua hivi karibuni, Dei-Tutu ameeleza juhudi za China kusaidia nchi za Afrika kuhusu suala la madeni kuwa ni chachu muhimu kwa maendeleo ya kasi katika maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu na kilimo. Amesema China imeendelea kuwa mwenza wa dhati wa maendeleo kwa nchi zinazoendeleza zinazohitaji mitaji mikubwa katika miradi mbalimbali, na kuongeza kuwa China daima imeshikilia kanuni ya usawa katika uhusiano wa pande mbili, na kushiriki kivitendo katika majadiliano ya usawa na haki na nchi tofauti ili kukabiliana na masuala kama hayo.

Amepinga vikali kile kinachoitwa mtego wa madeni, akisema mikopo inayotolewa na China inazivutia nchi za Afrika na nchi nyingine zinazoendelea kutokana na kuwa na unyumbufu, na kuongeza kuwa, suala la madeni ya Afrika linahitaji juhudi za pande zote.