Rais wa Tanzania awahimiza maofisa wa kikanda kuhakikisha usalama wa chakula
2023-08-28 08:41:27| cri


 

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, jana amewahimiza wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa kuhakikisha usalama wa chakula katika maeneo yao.

Akizungumza kwenye hafla ya kufunza mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala yaliyofanyika kwa siku 6 katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, rais Samia amesema, maofisa hao wanapaswa kuwahimiza vijana kushiriki kwenye kilimo ili kuhakikisha nchi hiyo ina chakula cha kutosha.

Vilevile amewataka kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambayo inapaswa kutekelezwa kwa vigezo vilivyowekwa, na kuwataka kusuluhisha migogoro ya ardhi, na kusikiliza na kutatua malalamiko ya wananchi katika maeneo yao