Watu 23 wauawa katika mapigano kati ya jeshi la serikali ya Yemen na waasi wa kundi la Houthi
2023-08-28 08:41:01| cri

Watu 23 wameuawa katika mapigano makali kati ya jeshi la serikali ya Yemen na waasi wa kundi la Houthi katika mkoa wa Lahj kusini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la serikali katika jimbo la Lahj, Bw. Mohammad Najib, amesema, waasi hao jana walifanya mashambulio ya ghafla dhidi ya maeneo yaliyolengwa ya jeshi la serikali katika jimbo hilo, na kusababisha majibizano makali ya risasi kati ya pande hizo mbili. Mapigano hayo yalisababisha vifo vya waasi 15 wa kundi hilo na wanajeshi wanane wa serikali, na wengine 10 kujeruhiwa.

Kundi la Houthi halijatoa tamko lolote kuhusu mapigano hayo.