Ushirikiano wa dhati kati ya Afrika na China umepata manufaa ya kidhahiri
2023-08-29 08:35:50| CRI

Mtaalamu wa masuala ya uhusiano wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Ufundi nchini Angola, Osvaldo Mboco amesema, ushirikiano wa dhati kati ya nchi za Afrika na China umepata matokeo chanya na yanayoonekana kidhahiri, ambayo yanachochea manufaa na maendeleo ya pamoja.

Mboco amesema, katika ushirikiano wake na Afrika, China pia imejenga msingi bora wa miundombinu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii katika bara hilo, na kusaidia katika mapinduzi ya kiviwanda na kuimarisha thamani ya biashara katika bara hilo.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Mboco amesema, Angola kwa sasa imeibuka kama soko muhimu barani Afrika, na kushuhudia kampuni nyingi za China zikianzisha ama zikipanga kuanzisha viwanda vya uzalishaji nchini humo, na kuongeza kuwa kampuni hizo zinasaidia kutoa fursa za ajira kwa Waangola.