Somalia yatakiwa kulinda usalama uliopatikana wakati wa mpito
2023-08-29 08:35:16| CRI

Maofisa wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wameitaka Somalia kuhakikisha kuwa, usalama uliopatikana kwa nguvu kubwa mpaka sasa hautawekwa hatarini wakati vikosi vya Umoja wa Afrika vikiendelea kuondoka nchini humo.

Kaimu mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Afrika Zinurine Alghali ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha juhudi zilizotumika kuleta utulivu hazitapotea bure. Amerejea tena ahadi ya Umoja wa Afrika ya kuhakikisha Somali inabeba wajibu kamili wa usalama ili kuhakikisha utulivu, maendeleo, na ustawi kwa watu wake.

Naye mkuu wa Ofisi ya Usaidizi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOS) Aisa Kirabo Kacyira amethibitisha ahadi ya Umoja huo ya kuhakikisha mpito wa utulivu na kupongeza wadai kwa mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya kupunguza vikosi vya  Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) nchini humo.