China yasema kuongeza wanachama katika kundi la BRICS kutaongeza sauti ya nchi zinazoendelea kwenye mambo ya kimataifa
2023-08-29 09:36:05| cri


 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, kuongeza wanachama katika ushirikiano wa BRICS kutaongeza sauti ya masoko yanayoibuka na nchi zinazoendelea kwenye masuala ya kimataifa.

Akizungumza jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Bw. Wang amesisitiza kuwa, lengo la ushirikiano wa BRICS ni kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja, hautajihusisha na mvutano kati ya makundi yanayopingana, na ushirikiano wa BRICS ni tofauti kimsingi na kikundi kidogo.