Mkuu wa jeshi la Sudan aahidi kutofikia makubaliano na kikosi cha RSF
2023-08-29 08:34:40| CRI

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan Jeneral Abdel Fattah Al-Burhan amesema kamwe hatafikia makubaliano na kikosi cha RSF.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza la Utawala la Mpito la Sudan, Jenerali Al-Burhan amesema hayo jana jumatatu wakati akizungumza na askari katika kambi ya jeshi la majini ya Flamingo katika eneo la kijeshi la mkoa wa Bahari Nyekundu mashariki mwa Sudan.

Amesisitiza kuwa jeshi la Sudan litaendeleza vita dhidi ya wapiganaji wa kundi la waasi, ambao wamewatishia wananchi, kukiuka imani zao, na kuiba mali na fedha zao.