Misri, Ethiopia na Sudan zaanza duru mpya ya mazungumzo kuhusu mgogoro wa Bwawa la Renaissance
2023-08-29 08:33:38| cri

Wizara ya Rasilimali ya Maji na Umwagiliaji ya Misri imesema nchi hiyo pamoja na nchi za Ethiopia na Sudan zimeanzisha duru mpya ya mazungumzo kuhusu suala la Bwawa la Renaissance la Ethiopia huko Cairo, Misri.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri, Bw. Hani Suweiram imesisitiza kuwa, ni lazima kwa nchi hizo tatu kufikia makubaliano ya kisheria ya kuhifadhi na kuendesha maji ya Bwawa la Renaissance, kwa kuzingatia maslahi na wasiwasi wa nchi hizo tatu, na kuhimiza kusitishwa kwa hatua za upande mmoja juu ya ujazaji na uendeshaji wa bwawa hilo.

Pia amesisitiza kuwa, kujaza na kuendesha bwawa hilo bila makubaliano ya pande tatu kunakiuka tamko la kanuni zilizosainiwa na nchi hizo tatu mwaka 2015.