Waziri wa Ulinzi wa China, Li Shangfu, ametoa wito wa kufanyika kwa juhudi za pamoja kati ya China na Afrika ili kuimarisha ushirikiano na kulinda usalama wa dunia.
Akitoa hotuba katika kikao cha tatu cha Jukwaa la Amani na Usalama la China na Afrika lililofanyika hapa Beijing jana, Bw. Li amesema ubinadamu umekabiliwa na changamoto ambazo hazijawahi kutokea wakati maendeleo ya dunia yakiingia katika zama mpya ya ukosefu wa utulivu na mageuzi. Amesema China iko tayari kuungana na Afrika kukabiliana na changamoto za kiusalama na kulinda uwiano wa haki ya kimataifa, hivyo kuongeza uhakika na utulivu zaidi duniani.
Zaidi ya wawakilishi 100 wa ngazi ya juu kutoka Umoja wa Afrika (AU) na nchi karibu 50 za Afrika walihudhuria mkutano huo, ambapo walitoa hotuba kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo amani na usalama, usalama wa baharini, na hali ya kupambana na ugaidi barani Afrika.