Kenya yatumia matamasha ya muziki na maigizo kutangaza utalii wa ndani
2023-08-30 08:35:19| CRI

Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB) imesema inatumia matamasha ya muziki kuchochea na kukuza utalii wa ndani ya nchi hiyo.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo John Chirchir amesema, soko la ndani ni sehemu muhimu yenye uwezo wa kudumisha sekta ya utalii nchini humo endapo itatumika vizuri kupitia njia mbalimbali ikiwemo matamasha ya muziki. Amesema Bodi hiyo imeingiza ajenda za utalii katika matamasha ya muziki yaliyomalizika hivi karibuni nchini humo, na kuvutia watu wengi.

Pia Bw. Chirchir amesema, wakati utalii wa kigeni unachukua nafasi muhimu katika kuingiza pato linalotokana na utalii, Bodi hiyo inaendelea kusisitiza umuhimu wa kuendeleza utalii wa ndani ili kuleta uwiano katika pato hilo.