Misri, Ethiopia na Sudan zashindwa kufikia makubaliano kwenye mazungumzo kuhusu bwawa la GERD
2023-08-30 08:33:20| cri

 

Wizara ya Raslimali ya Maji na Umwagiliaji ya Misri imesema, nchi hiyo, Ethiopia na Sudan zimemaliza mazungumzo kuhusu bwawa la GERD la Ethiopia, bila ya kufikia makubaliano yoyote.

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, lengo la mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 27, lilikuwa ni kufikia makubaliano kuhusu uhifadhi wa maji na kanuni za uendeshaji, lakini msimamo wa Ethiopia haukubadilika kwenye mazungumzo hayo.