Umoja wa Mataifa watoa wito wa dola bilioni 1 za kimarekani kusaidia watu wanaokimbia Sudan
2023-08-30 08:33:46| cri

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Bw. Filippo Grandi jana alitoa wito wa dola bilioni moja za kimarekani kusaidia waliorejea na wakimbizi waliokimbia mgogoro wa Sudan na kuelekea nchi jirani.

Bw. Grandi alisema katika mji mkuu wa Sudan Kusini wa Juba kwamba, kutokana na ongezeko kubwa la watu kutoka Sudan, UNHCR imemaliza rasilimali zote ilizokusanya hapo awali na sasa inahitaji fedha zaidi. Alibainisha kuwa kati ya fedha hizo, Sudan Kusini itapokea dola milioni 356 za kimarekani wakati zilizosalia zinaweza kwenda nchi nyingine kama vile Chad na Misri, ambazo pia zinapokea wakimbizi kutoka Sudan.