Tanzania yaongeza nguvu ya kupinga umiliki wa silaha kinyume na sheria
2023-08-31 08:26:03| cri


 

Mamlaka nchini Tanzania jana imetangaza hatua mpya kali dhidi ya umiliki wa silaha kinyume na sheria, na kuwataka wamiliki wa silaha hizo wazisalimishe kwa polisi ndani ya miezi miwili kuanzia tarehe 1 mwezi Septemba hadi tarehe 31 mwezi Oktoba.

Katika taarifa yake, Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamad Masauni amesema, wamiliki wa silaha kinyume na sheria ambao hawatasalimisha silaha hizo katika kipindi kilichotangazwa watashitakiwa.

Taarifa hiyo imesema, silaha haramu zinatishia usalama wa raia, na baadhi ya silaha hizo zinatumika kwenye matukio ya ujambazi wa kutumia silaha.