FAO yasema mvua za El Nino huenda zikawaathiri Wasomalia milioni 1.2 mwaka huu
2023-08-31 08:29:49| CRI

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema mvua za El Nino zinazokaribia kunyesha huenda zikawa na athari hasi kwa watu milioni 1.2 nchini Somalia mwaka huu.

Shirika hilo limesema katika mpango wake wa hivi karibuni uliotolewa mjini Mogadishu kuhusu kupunguza,  maandalizi na majibu kwa mwezi Agosti 2023 hadi Januari 2024, kwamba hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa ili kulinda uhai na maisha ya watu.

Kwa mujibu wa Shirika hilo, jamii zinazoishi kando ya mito ziko hatarini zaidi huku hekta karibu milioni 1.5 za ardhi zikiwa katika hatari ya kukumbwa na mafuriko, na kuongeza kuwa hatua za awali zinaweza kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.