IMF yasema nchi zilizo hatarini zaidi barani Afrika ndizo wahanga wakubwa wa mabadiliko ya tabianchi
2023-08-31 08:28:53| CRI

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limesema nchi zilizo hatarini zaidi barani Afrika na zile zinazokabiliwa na mapigano ndizo zinaathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi.

Katika ripoti yake iliyotolewa jana jumatano, IMF imesema nchi zilizo hatarini, hali mbaya ya hewa pamoja na mapigano, utegemezi mkubwa wa kilimo cha mvua, na uwezo mdogo wa kusaidiana vinaongeza athari hasi kwa maisha ya watu na uchumi.

Ripoti hiyo imesema msaada endelevu wa kifedha kutoka wenzi wa maendeleo wa kimataifa unahitajika ili kukwepa hali ya njaa na mapigano kuwa mbaya zaidi, jambo litakalochochea uhamaji wa nguvu wa watu na uhamiaji.

Shirika hilo limezitaka nchi dhaifu za Afrika kutekeleza sera ili kuwezesha majibu ya haraka ya athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia hatua kama ujenzi wa kinga katika bajeti na kuwa na hifadhi ya fedha za kigeni.