China yatoa wito wa kulindwa utaratibu wa kimataifa wa usalimishaji wa silaha
2023-08-31 08:30:21| cri

Mjumbe wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Ren Hongyan ametoa wito wa kudumishwa kwa utaratibu wa kimataifa wa usalimishaji wa silaha na kupinga mawazo ya vita baridi na mvutano kati ya kambi.

Akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha "Siku ya Kimataifa ya Kupiga Marufuku Majaribio ya Nyuklia", Balozi Ren amesema, mfumo wa kimataifa wa udhibiti wa silaha, usalimishaji wa silaha na kutosambaza silaha unakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiwa, na hatari za mbio za silaha za nyuklia na migogoro ya nyuklia zinaongezeka mara kwa mara. Amesema kutokana na hali hii, ni lazima kutekeleza kwa uthabiti ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, na kushikilia taratibu za kimataifa za usalimishaji wa silaha, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Kupiga Marufuku ya Majaribio ya Nyuklia, kupinga mawazo ya Vita Baridi na mvutano kati ya kambi, na kufanya jitihada zaidi katika kuzingatia ustawi wa binadamu wote na kufikia usalama wa pamoja.