Tume ya AU nchini Somali yaitaka jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mchakato wa kujenga amani ili kuleta utulivu nchini Somalia
2023-09-01 08:35:12| CRI

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuunga mkono mchakato wa kuleta utulivu nchini Somalia.

Kamanda wa Kikosi cha ATMIS Bw. Sam Okiding amesema dunia inapaswa kuunga mkono juhudi za kujenga amani katika maeneo muhimu, ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo vya silaha, kujenga uwezo, kutuma viwezeshaji nguvu muhimu, na utoaji wa fedha wenye uhakika na endelevu kwa ATMIS na serikali ya Somalia. .

Bw. Okiding amesema vikosi vya AU vimedumisha mafanikio yaliyopatikana kwa miaka mingi kwa kutopoteza eneo lolote kwa al-Shabab katika sekta zote, na hivyo kufikia jukumu la kulinda raia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kibinadamu nchini Somalia.

Bw. Okiding pia amethibitisha dhamira ya ATMIS ya kusaidia mashambulizi yanayoendelea kuongozwa na Somalia dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab ili kuhakikisha amani na usalama nchini Somalia kabla ya kuondoka kwake Desemba 2024.