Kenya yahitaji dola milioni 229 za kimarekani kwa ajili ya kukabiliana na ukame
2023-09-01 08:33:30| cri

Mamlaka ya Taifa ya Kudhibiti Ukame ya Kenya (NDMA), imesema, Kenya inahitaji shilingi bilioni 33.29 (dola za Marekani milioni 229) kwa ajili ya kukabiliana na ukame katika maeneo ambako baadhi ya watu milioni 2.8 bado wanakabiliwa na njaa.

NDMA imesema katika ripoti ya tathmini kwamba fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya msaada wa chakula, utoaji wa maji, maandalizi ya kukabiliana na El Nino, na uhifadhi wa wanyamapori ili kupunguza migongano kati ya wanyama na binadamu, ujenzi wa amani, na msaada wa ufufuaji wa shughuli za uchumi baada ya ukame.