Rwanda yaanza kukabiliana na dawa haramu za kuua wadudu kwenye kilimo
2023-09-01 09:30:01| cri

Serikali ya Rwanda inachukua hatua muhimu kutekeleza sheria, kufuatilia kwa karibu shughuli za mashambani, na kukuza mbinu endelevu za kilimo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na matumizi ya dawa haramu za kuua wadudu kwenye kilimo.

Maofisa wa Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Rwanda (REMA) wamezungumzia umuhimu wa mipango hii wakati wa mkutano wa mashauriano na uhamasishaji wa wadau kuhusu dawa zenye hatari zaidi (HHPs) uliofanyika juzi.

Mkutano huo ulioandaliwa na Mtandao wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo ya Rwanda (RCCDN), Chama cha Wanaikolojia wa Rwanda, na Mtandao wa Kimataifa wa Kutokomeza Uchafuzi (IPEN), umetoa jukwaa kwa wadau mbalimbali wa kilimo kujadili kuenea kwa dawa hizo na hatari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi yake.