China kuandaa Mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa kuhusu “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (BRI) mwezi Oktoba
2023-09-01 08:33:52| cri

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China itaandaa Mkutano wa kilele wa tatu wa ushirikiano wa kimataifa kuhusu pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” mwezi Oktoba hapa Beijing ikiwa ni moja ya shughuli muhimu za kuadhimisha miaka 10 tangu pendekezo hilo kutolewa, na pia kuzileta pande mbalimbali kujadili ujenzi wa sifa ya juu wa ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia moja”.

Bw. Wang amesema China inafanya mawasiliano na pande mbalimbali kuhusu maandalizi ya mkutano huo.