Bajeti ya sasa ya serikali ya Tanzania ni ya kujitegemea kwa asilimia 70
2023-09-01 09:29:33| cri

Tanzania sasa inaweza kugharamia bajeti yake kwa karibu asilimia 70 kufuatia mageuzi ya kodi ikiwa ni pamoja na kuimarisha usawa na ufanisi, kusisitiza ulipaji kodi wa hiari, kuendeleza mifumo ya kodi inayohimiza ukuaji wa uchumi na kushughulikia baadhi ya maswala ya kodi ya kikanda na kimataifa.

Akiongea mjini Dar es salaam kwenye ufunguzi wa mkutano wa 8 wa mtandao wa utafiti wa kodi wa Afrika (ARTN) uliowakutanisha wajumbe kutoka nchi 13, Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Philip Mpango amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuhakikisha kuwa kila fursa ya kodi inatumiwa kuzingatia hatua zinazoendelea za mapato na kuhakikisha utulivu katika soko, kutabirika na kusaidia ukuaji wa sekta binafsi na kukuza ari ya ujasiriamali.

Amesema Tanzania imeongeza usawa, uzingatiaji, ufanisi na kurahisisha mifumo ya kodi, na imeweka Mwongozo wa Kuboresha kodi unaojumuisha kuongeza elimu ya kodi na marekebisho ya sheria ili kushughulikia kutatua migogoro ya kodi na hivyo kupunguza urasimu katika kushughulikia rufaa za kodi.