China na Benin zaanzisha ushirikiano wa kimkakati
2023-09-02 08:19:45| cri

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Benin Patrice Athanase Guillaume Talon, wametangaza kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi zao.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya kufanyika kwa mazungumzo kati ya Rais Xi na Rais Talon, ambaye yuko ziarani nchini China.

Kwenye mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye jumba la mikutano ya umma, Rais Xi alibainisha kuwa katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya China na Benin umekuwa na maendeleo ya kasi, na maendeleo madhubuti yamepatikana katika ushirikiano. Ameongeza kuwa nchi hizo mbili zimesaidiana kwenye maswala yanayohusiana na maslahi ya kimsingi ya kila upande na yale yanayofuatiliwa na sana, na kudumisha mawasiliano ya sauti na uratibu katika mambo ya kimataifa.

Rais Xi amesisitiza kuwa China inashikilia umuhimu wa kuendeleza uhusiano kati yake na Benin, na iko tayari kudumisha mabadilishano katika ngazi zote, kuhimiza ushirikiano wa kirafiki na wenye faida katika nyanja mbali mbali, na kufiisha uhusiano wa nchi mbili kwenye kiwango kipya.